Alfagems Co. ltd

Secondary School

Morogoro Tanzania

Malengo ya shule

Nia ya kuanzisha shule yetu ni kuwapatia malezi na elimu ya sekondari hasa wasichana wanaoshindwa kuvipata sehemu nyingine kutokana na hali ngumu ya uchumi.

Kwa ajili hiyo, elimu inatarajiwa kutolewa kwa kudai tu karo iliyopangwa na serikali kwa ajili ya shule za binafsi, si zaidi. Kwa sasa ni 1/3 hadi 1/5 ya ada za shule nyingine za binafsi.

Shule yetu si kwa ajili ya watoto wa vigogo, bali ya matabaka ya chini, ili kuwapa watu wengi iwezekanavyo fursa ya kupata maendeleo na kuchangia ujenzi wa jamii yetu.

Shule yetu haiwabagui walengwa kwa msingi wa dini, wa kabila n.k.

Kati ya wanafunzi wapo watawa wa Kanisa Katoliki ili kuinua nidhamu na maadili, ambavyo vinazingatiwa sana.

Baadhi ya wanafunzi watakaofaa zaidi wataweza kuendelezwa na hatimaye kuajiriwa na kampuni kadiri litakavyohitaji.