Alfagems Co. ltd

Secondary School

Morogoro Tanzania

Mahali, Majengo na Huduma

Shule inaendelea kujengwa katika manispaa ya Morogoro, kata ya Kingolwira, mtaa wa Mji Mwema ambao mpaka sasa hauna shule yoyote ya sekondari.

Katika eneo linalomilikiwa na Jimbo Katoliki la Morogoro, sehemu inayokusudiwa kutumiwa katika ujenzi wa shule lina ukubwa wa eka kumi na moja hivi.

Kadiri ya ramani iliyoandaliwa, shule inatarajiwa kufikia idadi ya ofisi 9, vyumba vya madarasa 31, maabara 2, maktaba 1, ukumbi 1, nyumba za walimu 6, hosteli kwa wanafunzi 400, bwalo 2, matundu ya vyoo yasiyopungua 124 n.k.

Mpaka sasa zaidi ya nusu ya majengo hayo imekamilishwa. Kampuni linaendelea pia kutengeneza samani, pamoja na kununua vitabu na vifaa vya maabara vya kutosha.

Katika eneo hilo yameingizwa mabomba mengi ya maji safi kwa ajili ya wanafunzi.

Pia umeme wa Tanesco umeingizwa shuleni. Kwa dharura, lipo jenereta.

Usafiri wa daladala (Mjini-Mikese) unafika karibu na kituo.

Zahanati za binafsi zimejengwa jirani na eneo la shule.