Alfagems Co. ltd

Secondary School

Morogoro Tanzania

 

Uongozi wa shule

Shule yetu ni mali ya Jimbo Katoliki la Morogoro (S.L.P. 640 – Morogoro; www.morogoro.tk ). Siku za mbele inaweza ikaachwa moja kwa moja mikononi mwa Alfagems Co. Ltd., kampuni lililosajiliwa likiwa na makao makuu katika manispaa ya Morogoro, mtaa wa Kilakala, barabara ya Kilakala (S.L.P. 6083 - Morogoro).

Tangu sasa shule inaendeshwa na mmoja kati ya Wakurugenzi wa kampuni hilo (ambalo ni mali ya Jimbo kwa asilimia 80), akishirikiana na Mkuu wa Shule na walimu wengine pamoja na wawakilishi wa familia za wanafunzi kupitia Bodi ya Shule.

Shule inatarajiwa kuendelea kupata walimu wa kutosha wenye digrii au diploma, maadili, vipawa na juhudi za kuridhisha.

Hali ya kifamilia katika mafungamano, mvuto wa malengo maalumu ya kituo, na hakika ya malipo kwa wakati wake ni kati ya sababu zitakazowafanya walimu wapende kujiunga na shule.